Wednesday, January 27, 2016

Marahaba Swahili Music Festival 4th Edition 08 October 2016 Dar es salaam Tanzania

Marahaba Festival 

Mzuka-kwa-kwenda-mbele.

Mwimbaji-wa-Bendi-ya-nyimbo-za-asili-Isack-Abeneko-akiwa-ametala-jukwa-vya-kutosha.

Mashabiki wakifuatilia


Vikundi mbalimbali vya burudani

Natacha-akiimba-huku-akishikilia-bendera-ya-nchini-kwao.

Msani-wa-muziki-kutokea-nchini-Uganda-Muserebende-Hytham-Ssali-naye-akionesha-manjonjo-yake.


KAMPUNI YA MAGARI YA ALLIANCE AUTOS WAFANYA MAONYESHO NDANI YA JENGO LA GOLDEN JUBILEE TOWER (PSPF)

DSC_1573
Gari aina ya Amarok Pick up ikiwa katika maonyesho ya mauzo ndani ya jengo la Golden Jubilee Towers ambapo maonyesho hayo ambayo yanaenda sambamba na uuzwaji wa magari hayo yanaendelea hadi hapo kesho jioni kwa 'showroom' hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).
DSC_1562
Amarok Pick up inavyoonekana kwa ubavuni..
DSC_1563
Amarok Pick up inavyoonekana upande wa nyuma..
DSC_1566
Gari aina ya Touareg ambayo katika 'showroom' hiyo ya jengo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam kama inavyoonekana.
Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa kampuni ya magari ya Alliance Autos, ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen Tanzania (VW), Sheikha Said amebainisha kuwa, maonyesho hayo ya magari na mauzo yaliyoanza jana 26 Januari, yanatarajiwa kufikia tamati siku ya kesho 28 katika jengo hilo la Golden Jubilee Towers.
"Magari yaliyo kwenye 'showroom' hii ya ndani ya jengo la Golden Jubilee Towers ni pamoja na Amarok Pick up na Touareg. Tumeyaleta karibu zaidi na wateja wetu wapate kuyaona na kujua uhalisia wa 'German Engineering'. Na pia waweze kujibiwa maswali yao yote yanayowatatiza, kujua uwezo wa VW katika barabara zote" ameeleza Meneja masoko huyo.

Sunday, January 24, 2016

Harusi ya Edwin Hamli na Bi. Isabella Mushi ilivyofana

???????????????????????????????????? 
Bwana harusi Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakipozi kwa picha mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe na kufuataia na hafla ya kukata na shoka kwenye ukumbi wa Water Front jijini Dar es salaam usiku huu, hafla hiyo imehudhuriwa na ndugu marafiki na jamaa wa maharusi katika kufanikisha.???????????????????????????????????? 
Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakivishana pete wakatia walipofunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe.????????????????????????????????????
baadhi ya wasimamizi wa harusi hiyo wakishiriki ibada ya harusi hiyo kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe jijini Dar es salaam.???????????????????????????????????? 
Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakipozi wakiwa na waimamizi wao mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe.???????????????????????????????????? 
Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakionyesha vyeti vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe.???????????????????????????????????? 
Chilumba akiwa na wageni waalikwa wengine waliohudhuria katika hafla hiyo.????????????????????????????????????
Kombe pamoja na wadau wengine wakiwa katika hafla hiyo.????????????????????????????????????
Maharusi Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakipozi kwa picha kwenye ukumbi wa Woter Front mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe???????????????????????????????????? 
Bi. Harusi Isabella Mushi na waalikwa wakicheza muziki kwenye ukumbi nwa Woter Front.???????????????????????????????????? 
Mdau Kombe akiserebuka pamoja na wageni waalikwa wengine katika hafla hiyo.???????????????????????????????????? 
Chilumba wa pili kutoka kulia na Hassan Mabuyu wa pili kutoka kushoto wakiserebuka kwa muziki.

Friday, January 8, 2016

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Afanya Ziara Jeshi la Zimamoto

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (wa pili kulia) akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi. Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha akimuongoza mara baada ya kumpokea.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha akimuonesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (hayupo pichani) kifaa maalumu kinachofungwa kwenye chumba kutambua tukio la moto kabla ya kuleta madhara makubwa na hupiga king'ora mara baada ya kuhisi tukio hilo. Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linataka majengo yote yafungwe kifaa hicho ili kukabiliana na madhara ya moto.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha (kulia) akitoa taarifa fupi ya utendaji kazi wa jeshi hilo pamoja na mafanikio kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga alipotembelea makao makuu ya jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akishauri jambo baada ya kupokea taarifa fupi ya utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ziara yake aliyoifanya ambapo pia alitembelea kituo kikuu cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam kuangalia vifaa na shughuli za jeshi hilo. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akipokea nyaraka kadhaa pamoja na taarifa fupi ya utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji toka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha katika ziara yake.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ziara yake katika kituo kikuu cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam kuangalia vifaa na shughuli za jeshi hilo. 
Kituo cha kupokea taarifa za majanga ya moto cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akiwa katika Kituo Kikuu cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Jesuald Ikonko akimuongoza.
Hapa akipata maelezo toka kwa mafundi wa karakana kuu ya Jeshi la Zimamoto Ilala Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga akipata maelezo ya namna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na jeshi hilo vinavyofanya kazi kwa baadhi ya vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akipata maelezo ya namna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na jeshi hilo vinavyofanya kazi kwa baadhi ya vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya ziara yake katika ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...