Thursday, November 19, 2015

Kampuni ya TTCL Yakisaidia Kituo cha Afya Buguruni Dar

Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imetoa msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia)  ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia)  ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa tatu kushoto)  akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada katika kituo cha afya cha Buguruni leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea na kushoto kwake ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.
KAMPUNI  ya Simu nchini Tanzania (TTCL) leo imekitembelea kituo cha Afya cha Buguruni cha jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali ya vifaa pamoja na dawa kwa ajili ya kukiwezesha kutimiza majukumu yake ya kuwahudumiwa wagonjwa mbalimbali wanaokitegemea kituo hicho.

Katika zoezi hilo, TTCL imekabidhi mashuka 100, Vyandarua 100, Maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai zinazokikabili kituo hicho kwa ajili ya kuwahudumiwa wakazi wa maeneo hayo kiafya.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemas Mushi alisema zoezi hilo ni mwendelezo wa kampuni hiyo katika kurejesha faida kwa wananchi ambao ni wateja wa kampuni hiyo. Alisema wanaamini msaada huo unaenda kuwahudumia wananchi ambao ndiyo wateja wa kuu wa huduma za TTCL.

"...Vifaa hivi vinakwenda kuwatibu wananchi ambao tunaamini ni wateja wetu, hivyo wakiwa na afya njema ndiyo furaha kwetu na kuendelea kushirikiana nao kihuduma. Huu ni utaratibu wetu wa kawaida kila tunapopata kidogo tunakirudisha kwa wananchi...leo tumetoa mashine, mashuka 100, vyandarua 100 na dawa ambazo zitasaidia kuboresha huduma kwa wateja wetu," alisema Meneja huyo wa TTCL.

Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Maofisa Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Buguruni (kushoto) akimshukuru Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada huo ambao ni pamoja na vifaa tiba.
Alisema wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na kituo hicho cha afya na hasa kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu ugonjwa ambao umekuwa changamoto kwa jiji la Dar es Salaam. 

Kwa upande wake, Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea ameishukuru kampuni ya simu Tanzania kwa ukarimu wao na kuamua kukisaidia kituo hicho kwani wamesaidia kutatua changamoto anuai zinazokikabili kituo hicho katika kutoa huduma za afya. Aliomba makampuni mengine kufuata nyayo za TTCL kusaidia kutatua changamoto za huduma za afya katika vituo vya afya na hospitali anuai kulingana na mahitaji ya maeneo husika.

Kituo cha afya cha Buguruni ambacho leo kimenufaika na msaada huo ndicho kilichoteuliwa katika eneo hilo kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu ugonjwa ambao ulilipuka hivi karibuni kwa baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam na ambapo madhara yake yaliziathiri baadhi ya jamii jijini hapa.

Huyu Ndiye Waziri Mkuu Mteule wa Tanzania, Athibitishwa na Bunge kwa Kura 258

Rais John Pombe Magufuli (kushoto) akimnadi, Kassim Majaliwa jimboni kwake enzi za kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015. Rais John Pombe Magufuli (kushoto) akimnadi, Kassim Majaliwa jimboni kwake enzi za kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteuwa Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano. Dk Magufuli ametegua kitendawili kilichotanda katika Watanzania wengi hasa wafuatiliaji wa masuala ya siasa. Kassim Majaliwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jina lake limetajwa muda huu katika Ukumbi wa Bunge Dodoma na Spika wa bunge hilo, Job Ndugai na kuahirisha kikao cha bunge kwa dakika 45 kwa ajili ya kuandaa utaratibu wa Bunge kuthibitisha jina hilo kwa kulipigia kura.

 Bahasa iliyobeba jina la Waziri Mkuu imewasilishwa na Mpambe wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Bunge huku ikiwa imefungwa kwa bahasha tatu tofauti na ikiwa imeandikwa kwa mkono na Rais mwenyewe hali inayoonesha kulikuwa na usiri mkubwa kuvuja kwa jina la mteuliwa kabla ya kutajwa hapo bungeni. Kassim Majaliwa kihistoria fupi alizaliwa Desemba 22, mwaka 1960. Majaliwa ndiye aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa serikali ya Rais Jakaya Kikwete iliyo mpisha Rais Dk. John Magufuli.

 Kitaaluma ni Mwalimu aliyepata elimu yake Chuo cha Ualimu Mtwara (Mtwara TTC) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kiongozi huyu pia mbali na kufanya kazi katika nafasi mbalimbali serikalini lakini alipitia Jeshi la Kujenga Taifa kambi ya Makutopora (JKT).

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitishwa Mbunge wa Ruangwa(CCM), Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Kassim Majaliwa amethibitishwa na Bunge baada ya kupigiwa kura na kupata jumla ya kura 258 za ndio ikiwa ni sawa na asilimia 73.5 ya kura zote.

Ni kura 91 tu ikiwa ni sawa na asilimia 25.5 ndiyo zilizomkataa kiongozi huyo mteule na kiranja wa mawaziri wajao. Jumla ya kura halali 351 zilipigwa katika zoezi hilo huku kura mbili zikiharibika.

 Akizungumza na wabunge kutoa shukrani Kassim Majaliwa alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuongoza Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kisha kumteuwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Waziri Mkuu huyo mteule anatarajiwa kuapishwa kesho Ikulu ndogo ya Chamwino mjini Dodoma zoezi litakaloanza saa nne kamili asubuhi.


Wednesday, November 11, 2015

Kampuni ya TTCL yakanusha madai ya TEWUTA, Yadai hayana ukweli wowote


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi akizungumza na vyombo vya habari Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam kujibu madai ya TEWUTA.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mazungumzo ya Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (hayupo pichani) alipozungumza na vyombo hivyo leo jioni. 
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imepinga madai yaliyotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania (TEWUTA) jana dhidi ya Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL na kufafanua kuwa madai hayo si ya kweli zaidi ya upotoshaji wenye nia ovu ya kufanikisha malengo binafsi na kutaka kuikwamisha jitihada za TTCL katika maendeleo.

Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam alisema madai yaliyotolewa na Chama cha TEWUTA dhidi ya Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL hayana ukweli wowote bali wahusika walilenga kuupotosha umma.

"Menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), inapenda kuujulisha Umma kuwa, madai yaliyotolewa na Chama cha TEWUTA dhidi ya Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL si sahihi. Hoja hizo zimejikita katika upotoshaji wenye nia ovu ya kufanikisha malengo binafsi ya wahusika na kukwamisha jitihada kubwa zinazofanywa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wa TTCL wenye nia na malengo ya kutekeleza mpango mkakakti wa kuiboresha na kuiimarisha Kampuni ya Simu Tanzania.

Akifafanua zaidi Meneja Uhusiano huyo wa TTCL alisema mwaka 2007 Kampuni ya Simu Tanzania ilifanya mabadiliko ya Muundo wa Kampuni ili kuendana na hali ya soko la Ushindani katika sekta ya mawasiliano na Muundo uliopo sasa ni ule uliopitishwa na kuanza Kutumika mwaka 2007 baada ya kuidhinishwa na kupitishwa na Bodi ya Wakurugenzi.

Alisema menejimenti mpya ya TTCL iliyoanza kazi Februari 2013 iliainisha changamoto mbalimbali za kibiashara na kutengeneza Mpango Mkakati utakaoletab mabadiliko ya kibiashara na kuongeza tija, huku ikizingatia mabadiliko ya Kibiashara na ushindani wa soko katika  sekta ya mawasiliano, Menejimenti iliomba na kupata kibali cha Bodi ya Wakurugenzi wa TTCL kumtafuta Mshauri mwelekezi kwa njia ya Zabuni ili kupitia na Kushauri juu ya Muundo Mpya wa Kampuni utakaoendana na Mahitaji ya Kibiashara na kuleta ufanisi.

Aliongeza kuwa matokeo ya Kazi ya Mshauri mwelekezi yamelenga kubadilisha muundo wa Kampuni, Muundo wa Mishahara na Muundo wa utumishi. Mpango huu wa Mabadiliko ya Kibiashara unategemewa kukamilika katika kipindi cha mwaka 2016. Aidha alifafanua kuwa muundo wa mishahara unaotumika hivi sasa ni ule uliopitishwa Mwaka 2007 baada ya Kubadilika kwa Muundo wa Kampuni kama ulivyoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi wa TTCL.

"...Mfumo huu uliiweka TTCL katika nafasi ya kukabiliana na soko la ajira kimaslahi. Mfumo huu wa Mishahara ulizingatia pia matakwa ya kisheria ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Namba 6/2004 zimeainishwa aina tatu za Mikataba ya Ajira. Yaani: Mkataba wa Ajira usiokuwa na Muda Maalumu (Unspecified period of time), Mkataba wa Ajira wa Muda Maalum (Fixed Employment contracts) na pia Mkataba wa Ajira wa kazi Maalum (Special Task)..."

"...Hivyo Muundo wa Mishahara uliopitishwa mwaka 2007 uliainisha madaraja ya malipo na viwango husika ikiainisha aina ya mkabata, Mkataba wa Ajira usiokuwa na Muda Maalum na Mkataba wa Ajira wa Muda Maalum. Katika muundo huu madaraja na ngazi za Mishahara zimegawanyika katika ngazi Kumi (10) kuanzia TTCL 1 (Ikiwa ndio Kiwango cha Juu) hadi TTCL 10 (Ikiwa ndio kiwango kidogo) Muundo huu uko wazi na ndio unaotumika kulipa mshahara ya wafanyakazi wote wa Kampuni ya Simu Tanzania. Hakuna ulipaji wa mishahara (Payroll) yoyote ya Siri inayotumika tofauti na hiyo iliyoainishwa," alifafanua Meneja Uhusiano huyo katika taarifa yake.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bwana Mushi akifafanua masuala mbalimbali katika mkutano huo na vyombo vya habari.
Akizungumzia kuhusu Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL alisema imekuwa na mchango mkubwa katika kusukuma maendeleo ya TTCL chini ya uenyekiti wa Dk. Enos Bukuku na baadae chini ya Mwenyekiti wa muda Jaji Joseph Sinde Warioba.

Aliyataja baadhi ya mambo mengi yaliofanywa na Bodi hiyo kuwa ni pamoja na kuondoka kwa Mbia Mwenza Bharti Airtel na pia kuishauri Serikali juu ya umuhimu wa kuondoka kwa Bharti Airtel ndani ya TTCL ili kuwezesha juhudi za dhati za kuifufua TTCL.

"..Bodi imetoa ushauri, miongozo na maelekezo kwa menejimenti, imeshiriki vikao vya majadiliano ya kuondoka kwa Bharti Airtel na kipekee, imefanya mawasiliano na ofisi za Serikali zikiwepo Ofisi ya Rais na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kusisitiza umuhimu wa Kuondoka kwa Bharti Airtel. Juhudi hizi zimechangia sana kusukuma swala hili ambalo kwa sasa liko katika hatua za mwisho...," alisema Bwana Mushi.

Bodi ya wakurugenzi ilipitisha uamuzi wa TTCL kuingia katika mradi ya mabadiliko wa mfumo wa kibiashara ili TTCL iweze kupanua mtandao wake na kuwa wa kisasa zaidi kuweza kutoa huduma mbalimbali kwa teknolojia ya kisasa (GSM, UMTS & LTE) zikiwemo huduma za simu za mkononi na mawasiliano ya data kwa ufanisi zaidi ili  Kampuni iweze kukabiliana na ushindani ulioko sokoni na kuongeza pato lake. Tayari sehemu ya mradi huo imekamilika (4G LTE) ya kutoa huduma ya data kwa kiwango cha juu katika sehemu ya maeneo kadhaa ya Dar es Salaam. Utekelezaji wa mradi utaendelea kwa sehemu zingine.

Kwa kushirikiana na Serikali Bodi inaendelea kutoa ushirikiano stahiki katika hatua za kuiboresha TTCL zikiwemo kuhakikisha TTCL inapata mtaji wa kutosha kuendesha shughuli za mawasiliano ndani na nje ya nchi kuweza kuendana na Sera za Taifa na kuboresha pato la Kampuni. Bodi imekua ikitoa mchango mkubwa kuhakikiksha Mkongo wa Taifa unaendeshwa  vizuri kwa kuwa na mawasiliano wakati wote. Aidha, sambamba na maamuzi ya Baraza la Mawaziri juu ya TTCL kumilikishwa Mkongo wa Taifa, Bodi ya Wakurugezi imetoa mchango mkubwa juu ya ufuatiliaji wa swala hili kwenye Wizara husika. Serikali kupitia wizara hya Mawasiliano iko katika hatua nzuri katika kukamilisha swala hili." Alieleza katika taarifa yake.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mazungumzo hayo.
Akizungumzia Kampuni ya Rubiem ambaye ni Mshauri mwelekezi aliyepatikana kwa kufuata taratibu sahihi za manunuzi ya Umma, alisema mchango wa kampuni hiyo katika mpango wa mageuzi kibiashara ni mkubwa na unaonekana dhahiri tofauti na madai yaliyotolewa.

"...Matokeo ya kazi yake yataanza kuonekana mwishoni mwa mwaka huu ambapo huduma na bidhaa mpya zitaingia sokoni. Mshauri huyu anatarajia kukamilisha kazi yake katika robo ya kwanza ya mwaka 2016. Ieleweke pia kwamba, hatua ya Menejimenti kumuongezea muda mshauri huyu hazihusishi gharama zozote za nyongeza nje ya mkataba wake wa kazi na TTCL.
Menejimenti ya Kampuniya Simu Tanzania TTCL inaomba kutumia fursa hii kuwajulisha Umma kwamba, hali ya Kampuni yao ni thabiti, utendaji wa kazi unaendelea vizuri na jitihada mbali mbali za kuboresha huduma zinaendelea kwa ufanisi mkubwa," alifafanua Bwana Mushi kwa wanahabari.

"...Menejimenti ya Kampuniya Simu Tanzania TTCL inapenda kuujulisha Umma kuwa, oja zote zilizotolewa na TEWUTA si za kweli, ni taarifa zilizopotoshwa kwa makusudi, zikilenga kufanikisha malengo binafsi na kukwamisha jitihada kubwa zinazofanywa na Wizara ya Sayansi na Mawasiliano, Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni, Menejimenti na Wafanyakazi wa TTCL wenye lengo la kuifanya Kampuni kutimiza kikamilifu Wajibu wake kwa Umma. Ieleweke pia kwamba, Muundo wa mishahara ya Watumishi wa Kampuni ya simuTanzania TTCL uko wazi na ndio unaotumika kulipa mshahara ya wafanyakazi wote wa Kampuni ya Simu Tanzania. Ofisi inayolipa mishahara ya wafanyakazi wote wa TTCL iko idara ya Fedha na kusimamiwa na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu. Hakuna Payroll yoyote ya Siri inayotumika tofauti na hiyo iliyoainishwa, hakuna posho zozote zinalipwa kinyume na utaratibu." alieleza Meneja huyo wa TTCL.

Monday, November 9, 2015

Kampuni ya TTCL Yawasaidia Watoto Vifaa vya Masomo Kituo cha Awali Lukema Vingunguti

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services baadhi ya vibao maalumu kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi wa darasa la awali.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services baadhi ya maboksi ya chaki kwa ajili ya kufundishia watoto wa darasa la awali ikiwa ni sehemu ya msaada kukisaidia kituo hicho. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi. Kulia pembeni ni Ofisa Uhusiano wa TTCL Amanda 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kulia) akiwagawia madaftari wanafunzi wa darasa la awali ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa kukisaidia kituo hicho. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kulia) akiwagawia madaftari wanafunzi wa darasa la awali ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa kukisaidia kituo hicho. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.
Wanafunzi wa darasa la awali wa kituo cha LUKEMA kinachomilikiwa na Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services kilichopo jijini Dar es Salaam wakifurahia madaftari waliyopewa na TTCL kwa ajili ya masomo. Miongoni mwa vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali na mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.
Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) na walimu na uongozi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services linalomiliki kituo cha awali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa darasa la awali wa kituo cha LUKEMA mara baada ya kukabidhiwa misaada mbalimbali ya vifaa vya masomo. Miongoni mwa vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali na mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi. Shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 80 inakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa vifaa vya masomo kwa wanafunzi wake.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kulia) akimkabidhi baadhi ya mikeka Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali la kituo hicho kama msaada.
Muonekano wa darasa hilo la awali kabla ya kukabidhiwa mikeka ya kukalia, awali wanafunzi hao walikuwa wakikaa chini. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (anayeandika ubaoni) akiwachemsha bongo wanafunzi wa darasa la awali wa kituo cha LUKEMA kwa maswali ya hesabu kabla ya kukabidhi misaada ya vifaa vya masomo leo shuleni hapo.
Muonekano wa darasa hilo la awali baada ya kukabidhiwa misaada ya mikeka ya kukalia. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.

Saturday, November 7, 2015

JK Aondoka Rasmi Ikulu Kuelekea Kijijini Msoga Bagamoyo...!










Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli kuondoka rasmi Ikulu kabla ya kupanda chopa kuelekea kijijini Msoga Wilayani Bagamoyo kuanza rasmi mapumziko ya kustaafu wadhifa wake.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati akiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. Kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
  Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  wakati akiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
  Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Wakielekea kwenye helikopta itayowachukua hadi kijijini Msoga
 Picha ya pamoja kabla safari ya Msoga kuanza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu walimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho kikwete

Papa Wemba Awasili Dar, Aelekea Bagamoyo Kwenye Tamasha la Karibu Music Festival 2015

Mwanamuziki Papa Wemba (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie akimtambulisha kwa wenyeji wao.
Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.
Mapozi ya wanenguaji wa Papa Wemba katika picha mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la Karibu Music Festival 2015.
Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.
Msafara wa mwanamuziki Papa Wemba ukipokewa na wenyeji wao mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA).
Mwanamuziki Papa Wemba (kushoto) akiwa na Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie (kulia) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA).

Friday, November 6, 2015

Matukio Picha Hafla Rais Dk. Magufuli Kusherekea Kiapo Ikulu









 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli kwenye hafla maalum mara baada ya kuapishwa iliyofanyika Ikulu.
 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheim

  Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
  Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Hadija Mwinyi akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli.
  Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Sitti Mwinyi  akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
  Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Salma Kikwete  akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
  Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama  Asha Suleiman Iddi akifuatiwa na mkewe Mama Janet Magufuli
 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakiwa hema kuu
 Mama Janet Magufuli akisalimiana na Makongoro Nyerere
 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana na Makongoro Nyerere
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makongoro Nyerere
 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli  akiongea na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akienda kusalimiana na wageni wake
  Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake.
 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mtera Mteule Livingstone Lusinde.
   Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake.
   Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea  kusalimiana na wageni wake
 Mama Janet Magufuli akiwa na wageni wao

 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
  Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake

   Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na kutaniana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana kutniana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mhe Augostino Lyatonga Mrema wakati akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake. Hapa akiongea na Mbunge wa Morogoro vijijini mteule Mhe Propser Mbena
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake. 
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake. Hapa akiteta jambo na kijana George Mathias Mgina
 Rais Dkt Magufuli akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda na Mzee Joseph Butiku
 Mama Janet Magufuli akiamkia na na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo pinda wakiwa Rais Dkt Magufuli na Mzee Joseph Butiku
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janet Magufuli wakiwa na kijana George Mathias Mgina
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Tunu Pinda akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo pinda na wanafamilia
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na wake wa viongozi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Mizengo Pinda
 Mama Janet Magufuli akisalimiana na Mama Hasina Kawawa
    Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mhe Ole Sendeka
 Balozi wa Tanzania nchiniNigeria Mhe Njoolay akiwa na Mhe Chiligati na Mhe Profesa Jumanne Maghembe
 Wadau wakifurahia mchapalo
 Wadau wakiwa katika mchapalo huo
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Saidi Mwambungu na Mbunge Mteule wa Nyasa
 Blogger maarufu Haki Ngowi (kushoto) na nduguye ambaye ni mbunifu wa mavazi wa mkimataifa Sheria Ngowi ndani ya nyumnba
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake. Hapa ni rafiki yake na Waziri Mkuu wa Zamani wa Kenya Mhe Raia Odinga na ujumbe wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
   Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kusalimiana na wageni wake
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Salma Kikwete na familia ya Rais Mstaafu
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimianana na Mufti Mkuu wa Tanzania 
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipozi na viongozi wa BAKWATA
  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimaiana na viongozi wa dini

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na msanii Mrisho Mpoto

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

 Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni wake

  Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana  na wageni wake
Yamoto Band ikitumbuiza. Picha zote na IKULU

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...