Thursday, November 19, 2015

Huyu Ndiye Waziri Mkuu Mteule wa Tanzania, Athibitishwa na Bunge kwa Kura 258

Rais John Pombe Magufuli (kushoto) akimnadi, Kassim Majaliwa jimboni kwake enzi za kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015. Rais John Pombe Magufuli (kushoto) akimnadi, Kassim Majaliwa jimboni kwake enzi za kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteuwa Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano. Dk Magufuli ametegua kitendawili kilichotanda katika Watanzania wengi hasa wafuatiliaji wa masuala ya siasa. Kassim Majaliwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jina lake limetajwa muda huu katika Ukumbi wa Bunge Dodoma na Spika wa bunge hilo, Job Ndugai na kuahirisha kikao cha bunge kwa dakika 45 kwa ajili ya kuandaa utaratibu wa Bunge kuthibitisha jina hilo kwa kulipigia kura.

 Bahasa iliyobeba jina la Waziri Mkuu imewasilishwa na Mpambe wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Bunge huku ikiwa imefungwa kwa bahasha tatu tofauti na ikiwa imeandikwa kwa mkono na Rais mwenyewe hali inayoonesha kulikuwa na usiri mkubwa kuvuja kwa jina la mteuliwa kabla ya kutajwa hapo bungeni. Kassim Majaliwa kihistoria fupi alizaliwa Desemba 22, mwaka 1960. Majaliwa ndiye aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa serikali ya Rais Jakaya Kikwete iliyo mpisha Rais Dk. John Magufuli.

 Kitaaluma ni Mwalimu aliyepata elimu yake Chuo cha Ualimu Mtwara (Mtwara TTC) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kiongozi huyu pia mbali na kufanya kazi katika nafasi mbalimbali serikalini lakini alipitia Jeshi la Kujenga Taifa kambi ya Makutopora (JKT).

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitishwa Mbunge wa Ruangwa(CCM), Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Kassim Majaliwa amethibitishwa na Bunge baada ya kupigiwa kura na kupata jumla ya kura 258 za ndio ikiwa ni sawa na asilimia 73.5 ya kura zote.

Ni kura 91 tu ikiwa ni sawa na asilimia 25.5 ndiyo zilizomkataa kiongozi huyo mteule na kiranja wa mawaziri wajao. Jumla ya kura halali 351 zilipigwa katika zoezi hilo huku kura mbili zikiharibika.

 Akizungumza na wabunge kutoa shukrani Kassim Majaliwa alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuongoza Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kisha kumteuwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Waziri Mkuu huyo mteule anatarajiwa kuapishwa kesho Ikulu ndogo ya Chamwino mjini Dodoma zoezi litakaloanza saa nne kamili asubuhi.


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...