Monday, August 24, 2015

Samia Suluhu Aanzia Kampeni Kilimanjaro

[caption id="attachment_60986" align="aligncenter" width="620"]Mgombea mwenza wa nafasi ya uraisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu (katikati) akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo ya Same Mashariki (Anne Kilango-kulia) na Magharibi (David Matayo) Mgombea mwenza wa nafasi ya uraisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu (katikati) akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo ya Same Mashariki (Anne Kilango-kulia) na Magharibi (David Matayo)[/caption] [caption id="attachment_60984" align="aligncenter" width="800"]David Matayo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Magharibi. David Matayo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Magharibi.[/caption] [caption id="attachment_60985" align="aligncenter" width="710"]Anjela Kailuki Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania na Kamada wa Vijana wa Wilaya ya Same. Anjela Kailuki Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania na Kamada wa Vijana wa Wilaya ya Same.[/caption] [caption id="attachment_60982" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya wafuasi wa CCM wakimpokea Bi. Suluhu. Baadhi ya wafuasi wa CCM wakimpokea Bi. Suluhu.[/caption] Joachim Mushi, Same MGOMBEA mwenza nafasi ya uraisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu ameanza rasmi kampeni za kuomba ridhaa ya chama chake kupewa ridhaa na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kuongoza tena nchi. Samia ameanza ziara rasmi katika Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Same na kufanya mikutano ya hadhara katika Kata ya Hedari na baadaye wilayani Mwanga. Bi. Samia alilazimika kutembelea kituo cha Afya cha Hedaru na kuwasalimia wagonjwa na akinamama waliokuwa wakihudumiwa katika kituo hicho. Akihutubia katika mkutano wa Hedaru alisema anajua kero ya maji katika vijiji vya eneo hilo na tayari Serikali ya CCM imeanza kuifanyia kazi na kabla ya 2016/7 watakuwa wamepata maji kutoka eneo la nyumba ya mungu. Alisema ilani ya CCM imepanga kutoka shilingi milioni 50 kwa kila kijiji nchini hivyo kuwaomba wakichagu chama hicho. Alisema anatambua kero ya migogoro ya wafugaji na wakulima maeneo hayo hivyo wakipita yeye pamoja Mgombea Urais Dk. John Pombe Magufuli watahakikisha kero hiyobinamalizika kwa kupima ardhi ya eneo hilo ili kuonesha mipaka kuepuka migogoro. [caption id="attachment_60979" align="aligncenter" width="800"]Mgombea Mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akipokelewa katika Kituo cha Afya Hedaru kabla ya kuhutubia wananchi. Mgombea Mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akipokelewa katika Kituo cha Afya Hedaru kabla ya kuhutubia wananchi.[/caption] [caption id="attachment_60980" align="aligncenter" width="800"]Mgombea Mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa katika Kituo cha Afya Hedaru kabla ya kuhutubia wananchi. Mgombea Mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa katika Kituo cha Afya Hedaru kabla ya kuhutubia wananchi.[/caption] [caption id="attachment_60981" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya akina mama wakipata huduma katika kituo cha Afya cha Hedarua. Baadhi ya akina mama wakipata huduma katika kituo cha Afya cha Hedarua.[/caption] [caption id="attachment_60975" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya wafuasi wa CCM wakimpokea Bi. Suluhu ofisi za CCM Mkoa Kilimanjaro. Baadhi ya wafuasi wa CCM wakimpokea Bi. Suluhu ofisi za CCM Mkoa Kilimanjaro.[/caption] [caption id="attachment_60973" align="aligncenter" width="800"]Mmoja wa Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, akimvisha skafu Bi. Suluhu ofisi za CCM Mkoa Kilimanjaro. Mmoja wa Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, akimvisha skafu Bi. Suluhu ofisi za CCM Mkoa Kilimanjaro.[/caption] [caption id="attachment_60976" align="aligncenter" width="800"]Msafara wa Bi. Samia Suluhu ukielekea Hedaru. Msafara wa Bi. Samia Suluhu ukielekea Hedaru.[/caption] Alisema kwa wakazi wa Jimbo la Same Mashariki anatambua kero ya barabara ya Mkomazi hivyo wakipata ridhaa watahakikisha kuwa barabara ya mkomazi inakamilika. Alisema ilani mpya ya CCM imepanga kujenga majosho na kutoa madawa ya mifugo kwa wafugaji ili nao waweze kunufaika na fursha kama ilivyo kwa wafugaji. Samia katika msafara wake ameongozana na Amina Makilagi Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Anjela Kailuki Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania na Kamada wa Vijana wa Wilaya ya Same, Bi. Ummy Mwalimu Mjumbe wa Kamati ya kampeni ya Kitaifa na viongozi wengine wa Chama wa Wilaya na Mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...