Thursday, April 28, 2011

JK amteua Mkurugenzi mpya TBC

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO AMEMTEUA ALIEKUWA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI-MAELEZO, CLEMENT MSHANA KUWA MKURUGENZI MPYA WA SHIRIKA LA HABARI TANZANIA (TBC) KUZIBA NAFASI ILIYOACHWA WAZI NA MKURUGENZI ALIEMALIZA MUDA WAKE, TIDO MHANDO. UTEUZI HUO UMEFANYWA JANA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE.

Katibu wa Bunge 'awaponda' wabunge wapya

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah


KATIBU wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Thomas Kashililah amesema wabunge wengi kutofahamu vema kanuni za uendeshaji wa Bunge, ndiyo chanzo cha mivutano na vijembe kutawala vikao vya Bunge la 10.

Kashililah alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hali hiyo pia inachangiwa na uwepo wa wabunge wengi vijana, umelifanya Bunge kuonekana kama la wanafunzi. Tangu kumalizika kwa vikao vya Bunge la 10, wadau na wananchi wamekuwa wakikosoa mambo yaliyokuwa yakifanyika wakati wa Bunge hilo.

Katika Bunge hilo, baadhi ya wabunge walionekana kwenda kinyume cha kanuni na kuzusha majibizano yaliyoambatana na vijembe bila kuheshimu kiti. Wabunge hao walikwenda mbali zaidi pale baadhi walipotaka milango ya ukumbi ifungwe ili wachapane makonde kufuatia kushindwa kuafikiana katika baadhi ya mambo.

Dk. Kashililah alisema Bunge la 10 mkutano wa tatu linapaswa kuwa na wabunge 357 na kwamba, waliopo kwa sasa ni 350 huku asilimia 70 wakiwa ni wageni na vijana, ambao hawana uzoefu na mijadala.

Hata hivyo, alisema kuwa yaliyotokea katika Bunge hilo hayakusababishwa na udhaifu wa Spika Anne Makinda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Pia, alisema kuwa Spika Anne alitumia busara na uzoefu wa hali ya juu katika kuweka sawa mambo yaliyokuwa yakijitokeza. Spika ana mamlaka ya kumsimamisha mbunge asihudhurie vikao 10, iwapo atakiuka kanuni, lakini hakufanya hivyo kwa kuwa wabunge wengi bado wanajifunza," alisema.

Alisema kanuni imeweka wazi kuwa Spika wa Bunge anaposimama, mbunge anayezungumza anapaswa kuacha kuongea na kukaa, lakini hilo lilikuwa likikiukwa. Alisema kuna wakati Spika Anne alikuwa akisimama kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali, lakini wabunge nao wanasimama kwa kutofahamu taratibu.

"Hivi katika bunge la namna hiyo, utatoa adhabu kwa watu ambao unajua wapo darasa la kwanza, na mwingine anaibuka na kusema funga mlango tupigane, hawa wanapswa kufundishwa," alisema Kashillilah.

Wednesday, April 27, 2011

Irani yatoa USD mil 1.2 kusaidia Kilimo Kwanza

Naibu Waziri Nyarandu

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Irani imepanga kutoa dola za kimarekani milioni 1.2 (dola milioni 1.2) kuisaidia Tanzania katika utekelezaji wa vitendo kampeni za Kilimo Kwanza.
Taarifa imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati Balozi Msaidizi wa Iran nchini Tanzania Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kuzungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lazaro Nyalandu.
Katika mazungumzo hayo yaliyojikita zaidi kuimarisha uhusiano mzuri kibiashara baina ya nchi hizo mbili, Nyalandu kwa niaba ya Serikali ya Tanzania ameishukuru Iran kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo amewakaribisha wawekezaji kutoka Iran kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia vema fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo.

JK aongoza maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano



Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete akikagua gwaride rasmi lililoandaliwa kuadhimisha miaka 47 ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuunda Tanzania.



Rais wa Tanzania, Jakawa Kikwete (wa pili kulia), Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk. Shein (wa pili kushoto), Mama Mwanamwema Shein (kushoto) na Makamo Rais wa Tanzania, Dk. Ghalib Bilal (kulia) wakifurahia jambo baada ya Chakula Ikulu Zanzibar. Picha zote kwa hisani ya Ikulu.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete jana aliwaongoza Watanzania kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kitaifa Zanzibar.

Sherehe hizo zilifanyika jana Uwanja wa Amaan  Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Rais alipigiwa mizinga 21 kabla ya kukagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama.

Baadhi ya Viongozi waliohudhuria ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Salmin Amour.



Friday, April 22, 2011

Dk. Shein akutana na Balozi wa Uingereza Tanzania


Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianne Corner, Ikulu Mjini Zanzibar Aprili 21, 2011. (PICHA KWA HISANI YA IKULU ZANZIBAR)
 

Thursday, April 21, 2011

Siku ya Malaria Duniani


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani itakayoadhimishwa April 29 mwaka huu mkoani Arusha. kushoto ni  Mkurugenzi Mwakilishi wa Huduma za Jamii katika Wizara hiyo, Dk. Donan Mbando. (PICHA NA MDAU MAGENDELA HAMISI)

Mwandishi wa habari ashinda Luninga ya kisasa


Meneja Masoko wa Kampuni ya Coca-Cola Tanzania, Christina Maina (katikati), akimkabidhi Luninga aina ya Soni, Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Guardian, Renatha Msungu, aliyoshinda katika mchezo wa bahati nasibu ya papo kwa papo, iliyochezwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwenye uzinduzi wa kampeni kubwa ya masoko inayoitwa 'Open Happiness' uliofanyika Dar es Salaam Aprili 21, 2011. Kushoto ni Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Dimeji Olaniyan. (PICHA NA MDAU DOTTO MWAIBALE)

Mkutano wa wakuu wa nchi za EAC


Aprili 19, 2011 jijini Dar es Salaam ulifanyika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) uliojadili masuala anuai. Pichani ni baadhi ya viongozi wakuu wa nchi hizo, kutoka kushoto ni; Rais wa Uganda, Yoweri Mseveni, Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Waziri Mkuu wa Rwanda, Bernard Makuza na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. Picha na mdau wa Blog ya HM.

Ndoa ya Abdillah Abdallah Keto na Halima Chande Ibrahim


Bw. Abdillah Abdallah Keto akimvisha pete ya ndoa mkewe Halima Chande Ibrahim, baada ya kufunga ndoa katika Msikiti wa Sinza Mugabe jijini Dar es Salaam Aprili 08, 2011. Sherehe ya ndoa hiyo ilifanyika Mwananyamala nyumbani kwa bibi harusi.

Wednesday, April 20, 2011

Rwanda watwaa U-Katibu Mkuu EAC


Waziri wa Afya wa Rwanda, Richard Sezibera amechaguliwa kuwa
Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), pichani akizungumza na baadhi wa maofisa wa Jumuia hiyo mara baada ya kuchaguliwa.Richard Sezibera (kushoto) akiwa na Barozi wa Rwanda nchini Tanzania, Fatma Ndagiza. Nafasi hiyo awali ilikuwa ikishikiliwa na Bakari Mwapachu. Picha na mdau wa HM.

Monday, April 18, 2011

JAMBO LEO MABINGWA NSSF CUP


Mdau Mkuu wa Blog ya Harusi na Matukio (kushoto) ambaye pia ni mchezaji wa Jambo Leo akiwa amepokea kombe la mashindano ya NSSF baada ya timu yao kulitwaa juzi, kulia ni kaptani wa Jambo Leo Said Mweshehe akiwa ameshika kitita cha sh. 3,500,000 baada ya kuzitwaa na kombe. 


TIMU ya soka ya Jambo Leo ‘Wagumu Star’ inayomilikiwa na kampuni ya Jambo Concepts Ltd, imetwaa Ubingwa wa Kombe la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuifunga timu ya NSSF katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Sigara Chang’ombe Dar es Salaam.

Katika mchezo huo mkali uliofanyika jana, timu ya NSSF ndio walio kuwa wa kwanza kupata bao dakika chache baada ya mchezo kuanza lakini muda mfupi baadae Jambo Leo ilisawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji wake Said Abdul na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilitoka uwanjani zikiwa na bao moja (1-1).

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta bao la kuongoza, lakini timu ya Jambo Leo ndio waliokuwa wa kwanza kuziona nyavu za NSSF kwani dakika ya 47 mchezaji wa Jambo Leo Stivin Waigaga aliipatia timu yake bao la kuongoza.

Mchezo uliendelea kuwa mkali kwani NSSF walikuwa wakitafuta bao la kusawazisha vhuku Jambo Leo wakitafuta lingine ili kuweza kujihakikishia ushindi, likini hadi mwisho wa mchezo timu ya Jambo Leo iliibuka na mabao mawili na NSSF moja.

Kwa ushindi huo timu ya Jambo Leo imejinyakulia kikombe cha mashindano hayo pamoja na fedha taslimu sh. 3,500,000. NSSF kama washindi wa pili wamejinyakulia sh. 2,000,000, huku washindi wa tatu timu ya Uhuru ikijipatia sh. 1,000,000.

Upande wa mpira wa pete kwa mashindano hayo timu ya Habari Zanzibar ndio imeibuka washindi na kupewa kikombe pamoja na fedha. jipatiameifunga Uhuru 1-0 matokeo ambayo timu ya Uhuru imeonekana kushukuru kwa kufungwa bao moja tofauti na walivyotegemea.

Timu ya Jambo Leo ambayo imekuwa ikigawa dozi ya mabao matatu mpaka saba kwa kila timu ambayo inakutana nayo, katika mashindano hayo kiasi cha kuogopwa; Jambo Leo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa mashindano hayo hadi imeingia fainali.

PICHA ZAIDI SIKU YA FAINALI CHEKI.



Baadhi ya wachezaji, mashabiki na wafanyakazi wa Jambo Leo wakipiga picha huku wanashangilia NSSF CUP baada ya kulitwaa kombe hilo.


Nahodha wa timu ya mpira wa Miguu wa Jambo Leo, Said Mweshehe akiwa amebebwa na wachezaji wenzake mara baada ya kukabidhiwa kombe la NSSF CUP.



Gari maalumu la Kampuni ya Jambo Leo lililoandaliwa kwa ajili ya kubeba kombe lililochukuliwa na timu ya mpira wa miguu ya Jambo Leo, likiwa linaandaliwa kabla ya kupakizwa kombe kuelekea makao makuu ya kampuni hiyo Samora.


Kombe la NSSF likiwa chini ya himaya ya Jambo Leo baada ya kukabidhiwa.

Saturday, April 16, 2011

Jiulize, ingekuwa vipi kama wewe ungelisoma hivi?

Hili ndio darasa letu, na haya ndio madawati yetu, maisha yanaendelea. Hili ni moja ya madarasa ya shule za msingi Tz vijijini.

Friday, April 15, 2011

Basi la Ngorika lapata ajali laua 9, lajeruhi 16

Basi la Ngorika likiwa limepinduka baada ya kupata ajali ya kugongana na daladala Makumira

Na Mwandishi Wetu
Arusha

WATU 9 wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa huku wanne kati yao wakiwa na hali mbaya, baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana na kupinduka katika eneo la Makumira wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye, alisema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya saa 12:30 asubuhi nje kidogo ya Mji wa Arusha.

Alisema ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota hiece lenye namba za usajili T 773 BGT lililokuwa likiendeshwa na Selemani Juma (30) mkazi wa Kijenge na basi la Ngorika aina ya Scania namba T
633 ANF lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, likiendeshwa na Emanuel Mchoro (30) mkazi wa Mwanga, Kilimanjaro.

Kamanda Andengenye alisema alisema ajali hiyo ilitokea baada ya haice kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake akiwemo mwendesha baiskeli, hata hivyo kabla hajalipita aliona basi la Ngorika likija kwa kasi ndipo alipoamua kuingia porini ili kujinusuru asigongane uso kwa uso na gari hilo.

Hata hivyo kabla dereva wa haice hajafika mbali akiiacha barabara basi la Ngorika lilimgonga ubavuni na kusababisha watu 9 waliokuwa ndani ya gari hilo kufariki dunia papo hapo akiwemo dereva wa basi la Ngorika.

Andengenye aliwataja marehemu hao kuwa ni, Kizo Rafael Ndosi (35) mkazi wa Arumeru, Patriki Temba (28), Samsoni Emanuel Minja (60), Hamisi Charles (30), Huruma Safiel (28) wote wakazi wa Usariver na John Kess (38) mkazi wa Majichai.

Wengine ni Emanuel Mchoro (30) mkazi wa Mwanga ambaye ni dereva wa Ngorika na Fatuma Msuya (35) mkazi wa Usariver ambaye ni mwanamke pekee aliyekuwa katika ajali hiyo pamoja na dereva wa
baiskeli aliyejulikana kwa jina moja la Elvisa.

Alisema mpaka sasa jeshi la polisi linamshikilia dereva wa gari ndogo (hiece) mpaka pale upelelezi utakapo kamilika. Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Salashi Toure alisema kuwa wamepokea majeruhi 16 ambapo kati ya hao mmoja amehamishiwa katika hospitali ya Seliani baada ya mapafu yake kuvujia damu nyingi.

Thursday, April 14, 2011

Jamani chekini hii "bora punda afe lakini mzigo ufike"

Hii ni rumbesa ya magari, hapa ni kazi tu.

JAMBO LEO YAIVUA GAMBA TIMU YA UHURU


Kikosi hatari cha Jambo Leo "Wagumu Star' kabla ya kuanza kwa pambano.

TIMU ya soka ya Jambo Leo ‘Wagumu Star’ jana imeibajua timu ya soka ya Uhuru inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ‘wazee wa kujivua gamba’ katika mashindano ya Kombe la NSSF yanayoendelea jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha vyombo vyote vya habari.

Katika mchezo huo ulofanyika jana kwenye uwanja wa Sigara (TTC) Chang’ombe, Jambo Leo imeifunga Uhuru 1-0 matokeo ambayo timu ya Uhuru imeonekana kushukuru kwa kufungwa bao moja tofauti na walivyotegemea.

Timu ya Jambo Leo ambayo imekuwa ikigawa dozi ya mabao matatu mpaka manne kwa kila timu ambayo inakutana nayo, katika mashindano hayo kiasi cha kuogopwa na kila timu.

Uhuru walionekana kucheza mchezo wa kujiami tangu mwanzo kwani wachezaji wake hasa golikipa alionekana kuchelewesha mipira mithiri timu yake imeshinda jambo ambalo liliwafanya vijana wa Jambo Leo kupunguza kasi kadri ya muda ulivyokuwa ukiyoyoma.

Hadi mapumziko Uhuru ilikuwa ikicheza kwa kujiami huku wakitarajia kumalizika kwa pambano hilo wakiwa sare ili wakabahatishe kwenye penati katika mchezo huo wa nusu fainali.

Kipindi cha pili vijana wa Jambo Leo waliishtukia janja ya wapinzani wao na kuanza kuongeza kasi ya mchezo na kuwachanganya kabisa vijana wa Uhuru na katika dakika ya 72, Aziz Mustafa alifunga goli la shuti kali lililomshinda mlindamlango wa Uhuru na kukubali yaishe.

Hadi mpira unamalizika Jambo Leo ilikuwa na goli moja huku Uhuru wakiambulia patupu. Jambo Leo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa mashindano hayo hadi imeingia fainali. Hata hivyo Uhuru walionekana kuridhika na matokeo hayo kwani walijua katika mchezo huo wangeliangushiwa mvua ya magoli kama ilivyokuwa kwa kila timu inayokutana na Jambo Leo.

“Tunashukuru mungu sisi tumefungwa goli moja wenzetu wamekuwa wakifungwa 3, 4, hadi 7, hivyo tumejitahidi kwa matokeo haya…tumewabana kweli kweli,” alisema mmoja wa wachezaji wa timu ya Uhuru alipozungumza na HM. Mashindano hayo yanaendeleoa tena leo.

Kikosi cha Uhuru katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa pambano hilo.


Mchezaji nyota wa Jambo Leo, Juma Pinto akichuliwa na mmoja wa wahudumu wa kikosi cha msalaba mwekundu (aliye chuchumaa) kabla ya kuanza kwa pambano lao.


Mchezaji hatari wa Jambo Leo, Julius Kihampa (kushoto) mwenye mpira akikabwa na wachezaji wawili wa Uhuru.


Kocha Mkuu wa Jambo Leo, Jerry Cotto akitoa maelekezo kwa mshambuliaji wake, Said Abdul mmoja wa wachezaji wake wakati mpira ukiendelea.



Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Leo (waliosimama) wakifuatilia mpambano. Kutoka kulia waliokaa ni mmoja wa Wakurugenzi wa Jambo Leo, Benny Kisaka akifuatilia mchezo huo kwa makini, Jerry (kocha) na mchezaji wa akiba Julian Msacky.


Kocha wa Jambo Leo (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake namna ya kuwavua gamba vijana wa Uhuru wakati wa mapumziko, wa kwanza kushoto ni mmoja wa wajumbe wa benchi la ufundi la Jambo Leo, Edson Kamukara. Picha zote na mdau wa Harusi na Matukio


Wednesday, April 13, 2011

Andengenye Cup yakabidhiwa vifaa na BAKWATA Arusha


Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Arusha, Abbas Mkindi Daruesh akimkabidhi Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye jezi pamoja na dawa katika ofisi kuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya ANDENGENYE CUP vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tano(500,000) mashindano hayo yanaendelea mjini hapa.



Haya Kamanda nakukabidhi na vingine hivi hapa, kazi kwako!
Ndivyo anavyoonekana akisema, Abbas Mkindi Daruesh wakati akikabidhi vifaa hivyo jana.
PICHA ZOTE NA MDAU JANETH MUSHI


Tuesday, April 12, 2011

Wilson Mukama Katibu Mkuu mpya CCM


Katibu Mkuu mpya wa CCM, Wilson Mukama

Wilson Mukama awa Katibu Mkuu CCM

 HATIMAYE kitendawili cha mageuzi mkubwa ya CCM kupata viongopzi wapya wa Kamati Kuu (CC) ya Chama hicho kimeteguliwa na sasa atakayeshika nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa ni Wilson Mukama, huku akisaidiwa na John Chiligati kama Katibu Msaidizi aliyekuwa mwenyekiti Itikadi na Uenezi wa uongozi uliojiuzulu.

Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Nape Mnauye, anaye kuwa Katibu wa Itikadi na Habari, January Makamba anayekuwa Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje wa CCM, Lameck Nchemba Mweka Hazina mpya, Asha Abdullah Juma anayekuwa Katibu Oganaizesheni, Vuai Ali Vuai anayeshika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Wajumbe wengine wanaoingia Kamati Kuu ya CCM ni Pindi Chana, Abdulrahiman Kinana, Zakhia Meghji, Abdullah Kigoda, Steven Wasira, Costansia Buhiye, William Lukuvi, Dk. Hussein Mwinyi, Dk. Maua Daftari, Samia Suluhu, Shamsi Vuai Nahodha, Omarry Yusufu Mzee, Prof. Makame Mbarawa, na Mohamed Khatibu.

Laurent Gbagbo akamatwa hotelini


Laurent Gbagbo akiwa chini ya ulinzi wa majeshi ya Umoja wa Mataifa baada ya kukamatwa kwenye hoteli moja ambamo alikuwa amejificha mjini Abidjan. Taarifa zaidi zinasema vikosi vya wanajeshi vinavyo mtii Alassane Ouatarra vimemkamata kiongozi huyo na sasa yupo chini ya ulinzi na amekabiziwa kwa majeshi ya Ouatarra.

Chadema Zanzibar wachoma moto muswaada wa kuanzishwa ZEC


Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Hamad Mussa Yussuf , akichoma moto mswada wa sheria ya kuanzisha Tume ya kurekebisha Katiba Tanzania wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar. Picha na mdau Hamad Hija, Zanzibar

Yanga Bingwa Ligi Kuu, Simba waanza kutimuana


Kikosi cha timu ya Yanga ya Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam

BAADA ya timu ya Yanga ya Dar es Salaam kutangazwa Mabingwa wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, hali imekuwa mbaya kwa
wapinzani wao wa jadi timu ya Simba na sasa wameanza kutimuana.

Simba imeamua kulifumua upya benchi la ufundi na kuwaondoa
wachezaji 15 katika orodha ya usajili wa Ligi Kuu ya Tanzania.
Akizungumza Dar es Salaam jana mmoja wa viongozi waandamizi wa
klabu ya Simba, amesema klabu hiyo imeona bora ifanye hivyo ili
kuinusuru timu hiyo.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kuna vitu vingi amevigundua kama
baadhi ya wachezaji kujiamini na kufanya kila wanachotaka kwa
faida zao huku wakiiumiza timu.

Alisema baada ya kuangalia kwa kina wamelibaini hilo hivyo kuamua
wawaache watafute timu nyingine za kucheza. "Nimegundua kuna watu
wapo kwa ajili ya maslai yao na si timu hiyo ni bora tuwaache
wafanye mambo yao na kwenda kuchezea timu wanazotaka wao," alisema
kiongozi huyo wa simba.

Alisema kuna baadhi ya wachezaji wamekuwa wakifanya vitu tofauti
na mikataba yao na bila ya kutambua kuwa mpira ndiyo maisha kwao.
"Tunavunja mikataba ya wachezaji wanne ambao walikuwa bado mwaka
mmoja hii yote tuiweke timu sawa...na kuondoa kirusi kilichopo
ndani ya timu inaaelekea kila msimu tutaendelea kufanya hivi hivi
kama tutaendelea kuwa nao," alisema.

Hata hivyo chanzo kingine cha habari kinasema baadhi ya wachezaji
wanaoachwa yumo mchezaji mkongwe wa timu hiyo, Mussa Hassan Mgosi,
Kelvin Yondani na Mohamed Banka.


Kombe la Ligi Kuu ya Tanzania Bara likiondolewa Uwanja wa Taifa baada ya Timu ya Simba kushindwa litwaa kama ilivyokuwa ikitegemewa.


Monday, April 11, 2011

Viongozi wa siasa wafanyabiashara maarufu kutekwa

Sheikh Yahya Hussein

Na Mwandishi Wetu

MNAJIMU maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein ametabiri kuwa viongozi wa siasa na wafanyabiashara maarufu watatekwa kuanzia Aprili 19 na kuendelea hadi mwezi Julai.

Utabiri huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na mnajimu huyo na kusambazwa katika vyombo vya habari. Hata hivyo hakuweka wazi kuwa ni viongozi gain watatekwa au kutaja watu au makundi ambayo yatawateka.

“Viongozi wa siasa na wafanya biashara maarufu wajichunge kutekwa nyara na kuibiwa, wao wenyewe na kufanywa kama bidhaa. Viongozi hao wachukue tahadhari nyakati zao za kutembea na wanaposafiri kwani pana uwezekano wasirudi,” alisema katika taarifa yake.

Akifafanua zaidi alisema kuwa utekaji nyara huo ni wa viongozi walioelezwa kwa makundi kama madiwani, wabunge na nyazifa nyingine wa juu na kuongeza wasijiamini wanaposafiri au wakiwa kwenye mikutano wasiwe peke yao na wawe na mipangilio ya tahadhari nyakati zote. Nyota pia zinalenga wake na masahiba ya viongozi hao mashuhuri.

Mwisho


Friday, April 8, 2011

Vurugu za kuchangia maoni ya Katiba Mpya


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. James Msekela.akizungumza na waandishi wa habari akitoa ufafanuzi kuhusiana na vurugu zilizozuka katika mkutano wa utoaji wa maoni ya Katiba mpya katika viwanja vya Bunge Dodoma.

 

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) akilinda eneo la ukumbi wa bunge baada ya kuwatawanya wananchi waliofika kutoa maoni katika mchakato wa kupokea maoni ya Katiba Mpya na kuzuka kwa vurugu baada ya ukumbi kuwa mdogo tofauti na umati wa watu waliofika.



Baadhi ya wananchi wengi wakiwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwa nje kusubiri utaratibu wa kuingia ndani ya ukumbi wa Pius Msekwa uliokuwa ukifanyika mkutano huo wa wazi.



Mbunge wa Arusha Mjini tiketi ya Chadema, Godbless Lema (wa kwanza kulia), Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Msekela (kulia) wakijadili jambo baada ya vurugu kuzuka nje ya ukumbi wa Pius Msekwa.

Maandalizi ya Fiesta, mapambano ya mashabiki wa timu nane kubwa za Ulaya

Serengeti Fiesta Soccer Bonanza katika picha


Brass Bend ya Polisi Dar es Salaam ikiongoza maandamano ya mashabiki mbalimbali wa timu nane kubwa Ulaya yakielekea kwenye viwanja vya Leaders Dar es Salaam Aprili 8, 2011.



Mashabiki wa Manchester United wa Dar es Salaam wakishangilia moja ya ushindi wa awali walioupata katika viwanja vya Leaders, kwenye Bonanza la Soccer (Serengeti Fiesta Soccer Bonanza)



Mashabiki wa timu mbalimbali katika bonanza hilo wakiangalia mipambano anuai, hapa wamezunguka moja ya viwanja vilivyotumika kwenye mpambano huo.



Baadhi ya mashabiki wa Real Madriad wakishangilia timu yao katika viwanja hivyo.



Baadhi ya mashabiki wa Barcelona wakiwa wamekula pozi na na shabiki wa Chelsea (wa pili kushoto).








Vikao vya bunge vyaendelea Dodoma


Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Clement Mshana baada ya kuzungumza na maofisa habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Mikoa na wakala mjini Dodoma.

Thursday, April 7, 2011

Ujenzi daraja la Kigamboni kuanza


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John Msemo (kulia) katika eneo la Kurasini Vijibweni Dar es Salaam,  kuhusu ujenzi wa Daraja la Kigamboni eneo hilo. NSSF  inatarajia kuanza ujenzi wa Daraja hilo mapema mwaka huu baada ya zabuni kutangazwa na kumpata mhandisi. Daraja hilo litagharimu zaidi ya bilioni 130 hadi kukamilika kwake. (PICHA NA MDAU TIGANYA VICENT WA MAELEZO)

Tuesday, April 5, 2011

Mchungaji Mwasapile afanya maajabu kwa kibaka


Mchungaji Mwasapile


Na Mwandishi Wetu,
Loliondo


MIUJIZA ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile wa Kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro juzi Ilijidhihirisha kijijini hapa baada ya mmoja wa wezi aliyechomoa pochi ya mgonjwa raia wa Kenya kusalimisha pochi hiyo kwa Mchungaji huku akidai anapigwa na watu asiowaona na kushindwa kuona.

Aprili 2, 2011 mmoja wa raia kutoka nchini Kenya aliibiwa pochi iliyokuwa na fedha za Kenya sh. 20,000, simu, hati ya kusafiria na vitambulisho mbalimbali hali iliyomlazimu kutoa taarifa ya wizi huo kwa Mchungaji Mwasapile akiomba msaada.

Baada ya kutoa taarifa hiyo Aprili 3, majira ya saa saba mchana mchungaji Mwasapila alitangaza kwa watu waliokusanyika kijijini hapo na kutaka aliyeiba arejeshe vitu hivyo  na kwamba  asipofanya hivyo fimbo ya Mungu itamuadhibu.

“Ndugu zangu wagonjwa, Kijiji cha samunge kimevamiwa na majambazi na wezi ambao wameanza kuwaibia watu, nawaomba walioiba vitu hivyo wavirejeshe na waondoke kwa amani katika Kijiji hiki haraka kabla Mungu hajaanza kuwaadhibu kwa mkono wake,” alisikika akiwatangazia wananchi.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati watu waliokuwa wamefurika wakianza kupata dawa ghafla vijana wawili wakiwa wamefuatana na mama mmoja ambae jina lake halikufahamika mara moja walifika eneo la Mchungaji Ambilikile anakotolea dawa na kuomba msaada wake kuhusu kijana aliyekuwa analalama kuwa anapigwa na ambao hawaoni.

Kufutia hali hiyo, mchungaji Mwasapile alimwambia Kijana huyo aliyejulikana kwa jina moja la Joseph asalimishe vitu vyote alivyoviiba na kisha ampe dawa na baada ya kutoa simu aina Black Berry, fedha Sh. 20,000 za Kenya, hati ya kusafiria sh. 80,000 za Tanzania mchungaji alimmwagia dawa na ghafla alianza kuona na kuacha kupiga kelele.

Imebainika kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Joseph (28) alikuwa ametokea mkoani Singida na Mama yake ambaye ni mchuuzi wa Chakula eneo hilo.

Monday, April 4, 2011

Dk. Migiro amtembelea JK Ikulu kwa mazungumzo


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha Rose Migiro (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam. Dk. Migiro alifanya mazungumzo na Kikwete ikulu Aprili 4, 2011. Picha na Mdau Fredy Maro.


Naibu Katibu Mkuu wa UN, Dk. Migiro akiwa katika picha ya pamoja na Rais Kikwete Ikulu ya Dar es Salaam,  Dk. Migiro aliambatana na maofisa wengine kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa. 

Wanaooteshwa kuvumbua dawa ya magonjwa sugu waendelea kujitokeza



Haya makubwa: Huyu naye ameibuka mjini Morogoro yeye anatoa kikombe kimoja kama dawa ya magonjwa sugu, anajulikana kama Fatma Said Senga (41) mkazi wa Kata ya Kichangani Morogoro. Hapa katembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Said Mwambungu na viongozi wengine, kikombe chake anauza kwa sh. 200. Haya kazi Kwenu wadau, geuzeni msafara kuelekea Mji kasoro Bahari.

Friday, April 1, 2011

Wakumbuka vita vya Tanzania na Uganda?


Miongoni mwa majengo ya awali ambayo Nduli Iddi Amin Dada aliyalipua nchini Tanzania kabla ya kuzuka kwa vita vya Tanzania na Uganda. Jengo hili lilikuwa kanisa eneo la Kagera, Tanzania. Mdau Mkuu wa HM alitembelea maeneo hayo hivi karibuni.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...