Friday, December 31, 2010

Jamani angalieni keki za ajabu kwenye harusi


Kwanza cheki hii



alafu utazame keki hii.



Kisha angalia keki hii kwa makini.


 Na baada ya hapo tazama nyingine hii



Na mwisho angalia aina hii ya keki. Kisha utakuwa umejifunza kitu fulani, jamani haya ni madoido ya kwenye harusi. Keki hizo zimetumwa na mdau Neema Mgonja.

Sasa ni Maji ya Lady Jay Dee

Lady Jay Dee akionesha maji ya kunywa ambayo yana jina lake yanayotolewa na
Mohamed Enterprises Limited, akiwa ni msanii wa kwanza kupata endorsement ya
aina hiyo nchini. Hafla hii imefanyika leo katika hoteli ya Paradise City jijini Dar.
Akiongea na waandishi katika hafla hiyo Jay Dee pia aliweka wazi mipango yake
kwa mwaka 2011 ikiwa ni pamoja na kufungua mgahawa uitwao 'Nyumbani
Lounge' karibu na Best Bite Restaurant maeneo ya Ada Estate pamoja na kutoa
albamu yake ya tano. Picha kwa hisani ya Blog ya Michuzi.

Thursday, December 30, 2010

Angalieni mgambo wa jiji 'wanapotafuta' chochote

 Mgambo wa Jiji la Dar es Salaam wanaponasa mzigo wa Mmachinga na kuushikilia, yaani kiama wanauza na wao.


"Haya jamani mzigo ndio huu sasa vipi tupige pasu nini?" Kama vile wanasema hivyo, lakini ukweli ni kwamba wamemweka mmoja wa Wamachinga chini ya ulinzi kwa mahojiano zaidi, kilichoendelea 'sijui'. Picha na mdau wa blog Dotto Mwaibale.

Harusi ya Simon Wambura na Suzan Kimei


Maharusi Simon Wambura na Suzan Kimei, wakiwa katika ibada ya ndoa yao, iliyofanyika Juni 02, 2010, katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam. Picha na Mdau Dotto Mwaibale


i

Harusi ya Shedrack Saggat na mkewe Cecy

Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Habari Leo, Shedrack Sagati akiwa na mkewe Cecy muda mfupi baada ya kufunga ndoa yao, jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari mpya wa TFF, Boniface Wambura alipoagwa


 Baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa Jambo Concepts Ltd, wachapishaji wa gazeti la Jambo Leo na Jambo Brand wakifanya ishara ya kugonganisha vinywaji vyao katika hafla fupi ya kumuaga Ofisa Habari Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Boniface Wambura ambaye alikuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo kabla ya kuitwa TFF. Kapuni ya Jambo Concepts ilimzawadia lap top mpya ya kisasa kwaajiri ya kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya kabla ya kuondoka katika kampuni hiyo. 


 Mdau Mkuu wa Blog ya Harusi na Matukio akigongesha vinywaji kumpongeza Wambura, katikati mwenye tai ni mwandishi mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe.


Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Concepts, Juma Pinto akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo (hawapo pichani) kwenye hafla ya kumuaga Wambura, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni hiyo, Benny Kissaka. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi za Jambo Concepts jijini Dar es Salaam.

Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Boniface Wambura (wa pili kushoto), ambaye
ameteuliwa kuwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
akikabidhiwa zawadi ya kompyuta ndogo iliyotolewa na uongozi wa Kampuni ya
Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), wakati wa hafla ya kumuaga Dar es
Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa JCTL, Juma Pinto, Meneja
Mkuu, Ramadhani Kibanike, Mkurugenzi, Benny Kisaka na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Perfect Solutions, Evance Aveva ambaye ni Mshauri wa JCTL. Picha zote kwa hisani ya Jambo Concepts Ltd.

Ndoa ya Hemed Bweno na Mwajuma Sadik

Wakiwa na nyuso zenye tabasamu ni Hemed Bweno na mkewe Mwajuma Sadick,baada ya kufunga ndoa, Februari 20, 2010, Mwananyamala Dar es Salaam na kufuatia sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika nyumbani kwa bibi harusi.
Picha na Mdau Dotto Mwaibale.

Hayati Mama Salome Augustino Mgonja

ILIKUWA NI DAKIKA, SAA, SIKU NA LEO NI MIAKA 7 TANGU MAMA YETU MPENDWA SALOME AUGUSTINO MGONJA, ULIPOTUTOKA DUNIAni.

TULIKUPENDA SANA LAKINI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI, UNAKUMBUKWA NA MUMEO AUGUSTINO MGONJA, WATOTO WAKO SEIF, HUMPHREY, FREDY, ROSE,CHRISTINA,NEEMA,GLADY NA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI.

MAMA TUNAKUKUMBUKA SANA LAKINI TUNAJUA KIMWILI HAUPO NASI ILA KIROHO TUKO PAMOJA,NA SIKU MOJA TUTAONANA.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA,
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
-AMIN
PICHA KWA HISANI YA FAMILIA YA MGONJA.

Tuesday, December 28, 2010

Jamani kuna watu wabunifu si mchezo

Angalia hii ni kadi iliyotengenezwa kwa picha za watu tena marafiki wa karibu, picha hii ilitumiwa mdau Edson Kamukara hivyo akaona si vibaya wadau wengine wakaona ubunifu huu.
Alitumiwa na hii pia, ni mithili ya mti wa Chrismas wa 'Kichina'.

Pongezi afandeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Mdau wa blog, Henry Kiungulia akiwa katika hafla alioandaliwa na wanafamilia yake kumpongeza baada ya kumaliza mafunzo ya Ofisa Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam. Picha kwa hisani ya wanafamilia.

Kifo cha Abuu Semuhando wa Twanga Pepeta.

   
Gari lililosababisha kifo cha Abuu likiwa limetumbukia mtaroni pembezoni mwa barabara.
 
                                                                                                      
                                                                                                                     
Baadhi ya watu wakitazama pikipiki ya Abuu Semhando ilivyoharibika muda mfupi baada ya ajali yake.
 
   
Abuu enzi za uhai wake akiwa na wanamziki wenzake kabla ya moja ya safari za nje ya nchi.

MCT ilipowanoa wanahabari waandamizi

Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali vya  habari waliohudhuria mafunzo ya usanifu habari iliyoandaliwa na Baraza la Habari nchini (MCT) na kufanyika Dodoma Desemba 17, 2010.
Wakili Cecillia Assey Marealle (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na mume wake Aggrey Marealle, Mkurugenzi wa Executive Solutions na mama yake, Hellen Assey (kushoto) baada ya kuapishwa kuwa wakili kwenye viwanja vya Karimjee hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Picha kwa hisani ya Executive Solutions.

Siku JK alipolicharanga gitaa Ikulu

Rais DK. Jakaya Kikwete akilicharaza gitaa wakati alipowaongoza wanafamilia nyumbani kwake  kumpongeza mkewe Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa na kutimiza miaka 47 Novemba 30, 2010.

Siku ya 'Send off' ya Josephine Ndossy

Victor Kilowoko (kulia) akiwa na mkewe Josephine Ndossy siku ya 'Send off' ya mkewe iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

DJ Frank kutoka U-DJ hadi U-MC


Kwa wahudhuriaji wa sherehe, hafla ama harusi mbalimbali waweza kuwa tayari wamekutana na mdau huyu, anayejulikana kama 'DJ Frank'. yeye jina kamili ni Frank Ernest na kazi yake ni u-dj. Lakini waweza usiamini sasa mdau huyu ni MC mzuri na anaendesha shughuli zake kwa mbwembwe hatari, utakuwa shahidi mzuri pale utakapo gongana naye kwenye shughuli moja. Blog ya Harusi na Matukio baada ya kugongana naye imefanya mazungumzo kwa kina, kaa tayari kuyapokea.


DJ Frank  akiwa katika moja ya sherehe.

Chrismas 2010 na misaada kwa yatima

Vodacom Miss Tanzania, Genevieve Emmanuel  akimkabidhi  ndoo ya mafuta ya kupikia, Joyce Haule mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha  Msongola Orphanage Trust Fund, kilichopo Mvuti, wilayani Ilala, Dar es Salaam. Aidha kampuni hiyo kupitia kampeni yake ya ‘Share n Care’ pia ilikabidhi  vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi  milioni mbili katika hafla iliyofanyika wakati wa Sikukuu ya Krismas. Picha kwa hisani ya Vodacom.

Baadhi ya watoto Yatima wanaolelewa na Kituo cha Mtakuja Orphancs and Vulnerable Children Center cha Kariakoo, Dar es Salaam, wakipata chakula kilichotolewa na Kampuni ya simu ya TTCL kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismas. Vitu vingine walivyopewa ni sabuni, mafuta ya kula. Picha kwa hisani ya TTCL

Ajali na Chrismas 2010 Dar


Wakazi wa jijini wakiangalia gari namba T 902 ACN, lililotumbukia katika mtaro siku ya Sikukuu ya Krismas juzi Mtoni Kijichi Dar esSalaam, katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa. Picha na mdau DOTTO MWAIBALE


Siku kampuni ya Tigo ilipokisaidia Chuo Kikuu cha Zanzibar

Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) akikabidhi msaada wa kompyuta 10 zenye thamani ya sh. milioni 12 zilizotolewa na Tigo kwa Chuo Kikuu cha Zanzibar, mwishoni mwa wiki. Wa tatu kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Mustafa Roshash na wengine wanaoshuhudia ni baadhi wa wanafunzi, walimu na wawakilishi wa Tigo. Picha kwa hisani ya Tigo

Sunday, December 26, 2010

Mambo ya shopingi ya Chrismas Mtaa wa Kongo Dar es Salaam

"Sijui ninunue hili au..!" Ndivyo anaovyoonekana kusema mkazi mmoja wa jiji akiangalia mapambo ya Chrismas juzi



 Miti ya Chrismas jamani, hii ni ya kichina

Jamani angalieni usafiri ulivyo karaha Dar es Salaam

Jamani angalieni usafiri ulivyo karaha Dar es Salaam, mwana dada akiingia kwenye daladala kupitia dirishani bila woga.

Naibu Waziri wa Maji Injinia Chizza akitembelea vyanzo vya maji Temeke

Naibu Waziri wa Maji, Injinia Christopher Chizza (wa pili kushoto) akikagua vyanzo vya maji vilivyopo Manispaa ya Tekeme Dar es Salaam hivi karibuni, anayemwelekeza mbele ni Meneja wa Mtambo wa maji Mtoni, Masud Omar. 



 Waziri na baadhi ya maofisa wa maji, na waandishi wakiangalia mtambo wa kuchanganya maji na dawa.

Meneja wa Mtambo wa Maji Mtoni, Masud Omar (kushoto) akimwelekeza jambo naibu waziri kwenye moja ya mitambo ya maji eneo hilo. Picha zote na Mdau Dotto Mwaibale.

Januari 5, 2009, ilikuwa ni kumbukumbu ya maisha kwa Dk. Tumaini Simon na mkewe

Dk. Tumaini Simon akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa yao Januari 5, 2009. Hii ni kumbukumbu ya kihistoria kwa wanandoa hawa. Picha na Mdau Dotto Mwaibale.



Mke wa Dk. Tumaini Simon akimvisha pete mumewe kanisani siku ya ndoa.

Januari 5, 2009, ilikuwa ni kumbukumbu ya maisha kwa wanandoa hawa

Bw. Joachim Rasiel akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa yao kanisani. Picha na Mdau Dotto Mwaibale.


Wakiwa na nyuso za furaha, Januari 5, 2009, ni Geofrey Swai akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa yao. Picha na Mdau Dotto Mwaibale.



Geofrey Swai akiwa na mkewe katika picha ya pamoja


Swai katika mapozi na wife nje ya kanisa baada ya kufunga ndoa yao.

Januari 5, 2009, ilikuwa ni kumbukumbu ya maisha kwa wanandoa hawa

 
Januari 5, 2009, ni kumbukumbu ya milele kwa wanandoa hawa. Pichani ni Bw. Furaha Mwangosi akiwa na mkewe baada ya kuunganishwa rasmi katika maisha ya ndoa. Picha na Mdau Dotto Mwaibale.



Januari 5, 2009, ni historia kwa Bwana na Bibi, Brighton Munyo. Pichani Brighton Munyo akiwa na mkwe baada ya kufunga ndoa Kanisa Kuu Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam . Picha na Mdau Dotto Mwaibale.

Januari 5, 2009, ilikuwa ni kumbukumbu ya maisha kwa wanandoa hawa

DK. Lazaro Kapela akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa yao Januari 5, 2009. Mdau Dotto Mwaibale.



Bw. Sweetbet Mashine akiwa na mkewe muda mfupi baada ya kufunga ndoa yao Januari 5, 2009. Picha na Mdau Dotto Mwaibale.

Harusi ni kumbukumbu ya maisha kwa wanandoa, wafuatao ni miongoni mwa wadau waliofunga ndoa Januari 5, 2009

Bw. Joseph Phillip akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa yao Januari 5, 2009. Hii ni kumbukumbu ya maisha kwa wanandoa hawa. Mdau Dotto Mwaibale.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...