.

Wednesday, October 7, 2015

DK. Shein Aendelea na Mikutano yake ya Kampeni Zanzibar

Mama Fatma Karume akishuka jukwaani baada ya kuwahutubia Wananchi na Wana CCM katika viwanja vya mpira bumbwini makoba wakati wa mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, mkutano uliofanyika katika Jimbo la Bumbwini Unguja.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Mama Fatma Karume baada ya kuwahutubia Wananchi na kumuombea Kura kwa Wananchi wakati wa Mkutano huo wa Kampeni katika Wilaya ya Kaskazini B uliofanyika viwanja vya mpira bumbwini makoba.
Umati wa Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya mpira bumbwini makoba wakihudhuria mkutano wa mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein. 
Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mhe Salim Turky (Mr White) akiwa katika mkutano wa mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya bumbwini makoba wakimsikiliza Mgombea.
Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Mhe Haji Omar Kheri akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa kampeni ya Mgombea wa CCM Dk Shein, katika viwanja vya bumbwini makomba na kumuombea Kura Dk Shein, ili kuendeleza amani na utilivu na Masendeleo ya Wazanzibar.
Kada wa CCM Balozi Amina Salim Ali akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika mkutano wa kampeni ya Mgombea wa CCM Dk Shein 
Baadhi ya Wagombea wa CCM wakifuatilia mkutano wa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika Wilaya ya Kaskazini B Unguja katika viwanja vya mpira bumbwini makoba.
Kijana wa CCM akitowa maelezo kwa Ishara kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa kutosikiwa wakati Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia mkutano huo na kutowa Sera za CCM kwa kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya kupata ridhaa za Wananchi kumpigia kura kuongoza kwa mara ya Pili katika nafasi yake hiyo ya Urais wa Zanzibar.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini na kueleza mafanikio yaliotekelezwa na Dk Shein, katika kipindi chake cha miaka mitano inayomalizika na kuelezea Ilani ya CCM kwa miaka mitano ijayo.
WanaChama wa CCM wakimshangilia wakatin wa mkutano huo wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar.
Msanii Msechu akitowa buridani kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, katika viwanja vya bumbwini makoba Unguja.
                                                                    Mchechu ndani ya Zenj 
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira bumbwini makoba Unguja na kuwataka wananchi kumpigia kura ya ndio kuiongoza Zanzibar kwa mara ya pili kuendeleza Mafanikio kwa Wananchi wa Zanzibar katika Sekta mbalimbali za Uchumi Zanzibar. 

Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakati akiwahutubia na kuelezea Ilani ya CCM ya Uchaguzi kwa miaka mitano ijayo.
Mwanachama wa CCM akifuatilia hutuba ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohame Shein, wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya bumbwini makoba Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha wagombea wa CCM nafasi za Ubunge katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya bumbwini makoba Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha wagombea wa CCM nafasi za Uwakilishi katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya bumbwini makoba Unguja.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk. Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha wagombea wa CCM nafasi za Udiwani katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya bumbwini makoba Unguja.
Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Shein, wakati akiwahutubia katika viwanja vya bumbwini makoba Unguja akiwa katika mikutano yake ya Kampeni Zanzibar. 
Viongozi wa CCM na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, wakiitikia dua iliokuwa ikisomwa na Mzee wa Kijiji cha Bumbwini Makoba baada ya kumalizikika kwa mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar katika viwanja vya Mpira Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


CHADEMA MONDULI WASEMA WAO WATAANZA NA ELIMU

Mgombea udiwani monduli mjini kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Izak Joseph akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Monduli juzi katika viwanja vya  soko la alhamis  wakati akizindua rasmi kampeni za mgombea huyo.
************
Wagombea Udiwani na Ubunge jimbo la Monduli kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wametaja sekta ya elimu kuwa moja ya vipaumbele watakapofanikiwa kushinda uchaguzi mkuu ujao.

Akihutubia mkutano wa kampeni mjini Monduli juzi, mgombea ubunge kupitia Chadema Julius Kalanga alisema elimu ni msingi wa maendeleo katika sekta zote kwa sababu ndio huzalisha wataalam na watendaji katika miradi yote ya maendeleo.


"Aliyekuwa mbunge wa Monduli, Mheshimiwa Edward Lowassa amefanya makubwa katika sekta ya elimu, siyo tu Monduli, bali eneo lote la jamii ya wafugaji wa Kimaasai ambao kihistoria walionekana kubaki nyuma kieleimu. Nitaendeleza yote," alisema Kalanga


Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni afya, miundombinu, mawasiliano, uwezeshaji na uimarishaji wa miradi midogo midogo kupitia vikundi vya ujasiriamali pamoja na uhamasiahaji wa umma kushiriki harakati za maendeleo kwa kupanga, kuchangia, kitekeleza na kusimamia miradi katika maeneo yao.


Kwa upande wake, mgombea udiwani kata ya Monduli mjini, Isack Joseph "Kadogoo" anayetetea nafasi yake aliahidi kuendelea kuwalipia ada wanafunzi wote watakaofauli kuendelea na elimu ya sekondari ndani yakata yake, lakini wazazi au walezi hawana uwezo wa kugharamia elimu yao.


"Tangu niwe diwani mwaka 2010 hadi sasa nimeshawalipia zaidi ya wanafunzi 75 wanaosoma shule mbalimbali za sekondari ndani na nje ya wilaya ya Monduli. Nitaendelea kufanya hivyo," alisema Joseph

Alisema awali alikuwa akitumia fedha zake binafsi kabla ya kuingiza programu hiyo katika mipango ya matumizi ya fedha za maendeleo ya kata ili kuwezesha mradi wa ada kwa wanafunzi kuwa endelevu kwa kila diwani atakayefuata badala ya kubaki jambo lake binafsi.

Mama Samia Suluhu Awasili Kigoma, Wananchi Wasimamisha Shughuli Kumlaki


Baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan Kata ya Igagala, Uvinza Mkoani Kigoma wakimtaka awasalimie kabla ya kuendelea na safari. Mgombea mwenza huyo wa CCM ameingia mkoani Kigoma kwa ziara ya kampeni kuinadi ilani ya CCM.

Baadhi ya Wananchi wakiwa wamesimama pemezoni mwa barabara kumlaki mgombea mwenza wa urais CCM alipokuwa akiwasili Mkoani Kigoma kufanya mikutano yake ya kampeni.

Mgombea mwenza akizungumza na wananchi waliomsimamisha njiani kuwasilisha kero zao.
Mgombea mwenza CCM, Mama Suluhu akiwa ameshikilia kadi na bendera za vyama vya upinzani alizokabidhiwa na vijana waliohama vyama vyao na kujiunga na CCM, alipokuwa akiwasili Mkoani Kigoma mwisho wa reli.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan Kijiji cha Mlyabibi, Mkoani Kigoma wakimtaka awasalimie kabla ya kuendelea na safari. Mgombea mwenza huyo wa CCM ameingia mkoani Kigoma kwa ziara ya kampeni kuinadi ilani ya CCM.
Wananchi na wanaCCM wakimshangilia mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili mkoani Kigoma kuanza ziara yake ya kampeni. Mama Suluhu kawasili mkoani Kigoma na kufanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Kigoma Kusini, Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili Uwanja wa Tarafa Mwandika mkoani Kigoma kuhutubia wananchi katika ziara yake ya kampeni mkoani humo.
Baadhi ya vijana waliohama kutoka chama cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na CCM wakiwa wamemnyanyua juu mmoja wa viongozi aliyewashawishi kujiunga na chama hicho mara baada ya kupokelewa na mgombea mwenza wa CCM kwenye mkutano wa kampeni mjini Uvinza Kigoma. Zaidi ya vijana 60 wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Kata ya Uvinza, Himid Kisobwe wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mama Samia Suluhu.
Vijana waliojiunga na CCM kutokea chama cha NCCR-Mageuzi wakishangilia mara baada ya kumpokea Mama Samia Suluhu katika mkutano wa hadhara. Zaidi ya vijana 60 wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Kata ya Uvinza, Himid Kisobwe wamejiunga na CCM na kupokelewa na Mama Samia Suluhu.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili Uwanja wa Tarafa Mwandika mkoani Kigoma kuhutubia wananchi katika ziara yake ya kampeni mkoani humo.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Community Center Jimbo la Kigoma Mjini.
Burudani baada ya mapokezi ya mgombea mwenza kuwasili mkoani Kigoma.
Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba (kulia) akisalimiana na mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili Uwanja wa Tarafa Mwandika mkoani Kigoma kuhutubia wananchi katika ziara yake ya kampeni mkoani humo.
Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia wanaCCM na wananchi katika Uwanja wa Community Center Jimbo la Kigoma Mjini.

Mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia wanaCCM na wananchi katika Uwanja wa Community Center Jimbo la Kigoma Mjini. Picha na www.thehabari.com/Kigoma.

Tuesday, October 6, 2015

HATIMAYE VIJIJI VINNE WILAYANI HANANG’ VIMEPOKEA HATI ZA HAKIMILIKI ZA KIMILA ZA ARDHI

  Mzee wa heshima akielezea historia ya umiliki wa ardhi miaka ya nyuma ukilinganisha na sasa.
 Wanakijiji wakifuatilia tukio la makabidhiano ya hati za hakimiliki za kimila za vijiji vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vilivyopo wilayani Hanang’.
 Makko Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa kupima mipaka katika vijiji husika
 
 Baadhi ya akina mama wa Kijiji hicho wakifuatilia tukio
 Eveline Mirai, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' alitoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa sababu mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa wameikubali.
 Laurent Wambura Meneja wa program ya ufugaji kutoka Oxfam aliwapongeza wakazi wa vijiji hivyo vinne pamoja na wananchi mmoja mmoja ambao nao walipokea hati zao siku hiyo.
 Mkutano ukiwa unaendelea huku wanakijiji wakifuatilia
 Mmoja wa wanakijiji akiongea wakati wa Shughuli hiyo ya kukabidhi hati
 Mgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel akizungumza kabla ya kukabidhi rasmi vyeti.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Mreru James Gejaru akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi ya kimila ya kijiji chake.
 Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha Dirma Agustino Majawa akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi ya kimila ya kijiji chake
 hati ya hatimiliki ya kimila
  Mwanakijiji akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi yake
 Mwanakijiji akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi yake
 Wananchi na viongozi wa Serikali ya kijiji  wakipitia kwa makini hati za hakimiliki za kimila za ardhi.
Sherehe zilipambwa na ngoma ya wa-Barbaig

Na mwandishi wetu
Wenyekiti wa vijiji vinne vya wilaya ya Hanang’ wamepokea hati za hakimiliki za kimila za ardhi ya vijiji vyao baada ya kuwa vimepimwa na wao kupewa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwa ufadhili uliotolewa na shirika la Oxfam kupitia shirika la Ujamaa Community Resource Team - UCRT.

Vijiji hivyo vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vimekabidhiwa hati hizo na katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kijiji cha Mureru na kuhudhuriwa na wakazi zaidi ya 100 kutoka katika vijiji hivyo vinne.

Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wa vijiji hivyo vinne, Mbisha Gicharoda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ming’enyi aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwapatia elimu ya matumizi bora ya ardhi na kuwasaidia kupata hati za hakimiliki za ardhi ya vijiji. "Sisi kama wafugaji tulikua hatujui thamani ya ardhi yetu, sasa tumeamka na kujua haki zetu na manufaa ya kuwa na cheti cha umiliki wa ardhi", aliongezea.

Aidha mwenyekiti huyo alisema vijiji vyao kupata hati za hakimiliki za ardhi itawasaidia kuwa na eneo la pamoja la malisho na itawasaidia kuwa na nguvu zaidi ya kuilinda ardhi yao na kuisimamia vyema hali ambayo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi.

Katika hatua nyingine, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' Bi Eveline Mirai aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwasaidia wakina mama wajane nao kupata hati za hakimiliki za maeneo yao iliyoenda sambamba na kusaidia vijiji hivyo vinne kupata hati za vijiji.

Eveline alitoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa sababu mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa wameikubali. “Mtakapoheshimu mipaka, hatutakua na migogoro ya ardhi” na akawataka wananchi wenye maeneo yao kuhakikisha wanapata hati za hakimiliki za maeneo yao ili wayamiliki kisheria.

Naye meneja wa program ya ufugaji kutoka Oxfam Laurent Wambura aliwapongeza wakazi wa vijiji hivyo vinne pamoja na wananchi mmoja mmoja ambao nao walipokea hati zao siku hiyo. "Ukilinda maeneo ya wafugaji maana yake ni kwamba umewahakikishia maisha yao, tunapenda kuona haki za wafugaji zinapatikana" aliongezea.

Wambura aliishukuru serikali hususani Halmashauri ya wilaya ya Hanang’ kwa ushirikiano mkubwa ambao wameutoa kufanikisha zoezi hili na akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa serikali kushirikisha mashirika na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa ugawaji wa maeneo ya ardhi za vijiji kwani wanapogawa vijiji wakati mchakato wa upimaji unaendelea ni hasara kwa mashirika hayo kwani aidha yanalazimika kuanza kazi upya au kushindwa kwa sababu tayari fedha zinakuwa zimetumika na tatizo kwa wananchi linakuwa halijatatuliwa.

Naye Makko Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa kupima mipaka katika vijiji husika.

Changamoto nyingine ni pamoja na udhaifu katika uongozi wa serikali ya vijiji ambazo huchelewesha mipango lakini pia kuchelewa kupata ripoti ya matumizi ya ardhi kutoka wizarani nayo ni changamoto.

Naye Mgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo, alipozungumza kabla ya kukabidhi rasmi vyeti hivyo alizitaja faida za kumiliki ardhi kisheria kuwa ni pamoja na ardhi ile huwezi kupokonywa na mtu kirahisi, utajua mipaka ya eneo lako ambayo huwezi kuingiliwa na mtu na vilevile inaweza kuwa rasilimali baadaye ukapata fedha kukuwezesha kufanya vitu vingine zaidi.

Akitolea mfano, John alisema "Mara nyingi wakina mama huwa wanakosa haki yao pale mume anapofariki, huwa ananyanganywa mali yote ikiwa ni pamoja na ardhi wakati anaachiwa watoto awatunze, lakini wanapokuwa na hati za hakimiliki hakuna mtu anayeweza kuwapokonya kirahisi."